Taarifa Kuhusu AppGallery na Faragha

Mara ya mwisho kusasishwa: Januari, 2020

AppGallery ni huduma inayotolewa na Huawei Services (Hong Kong) Co., Limited kampuni inayomilikiwa na Huawei iliyosajiliwa ndani ya Hong Kong (hapa ndani baadaye inarejelewa kama "nasi", "sisi", au "yetu"). Inakupatia jukwaa la usambazaji ambapo unaweza kuvinjari, kufikia, kupakua na kudhibiti programu za bila malipo na za kulipiwa.

Taarifa hii inaeleza:

1. Tunakusanya Data Gani Kukuhusu?

2. Tunatumia Data Yako Kivipi?

3. Tunahifadhi Data Yako kwa Muda Gani?

4. Tunagawiza Data Yako Kivipi?

5. Una Haki Zipi na Machaguo Yapi?

6. Utawasiliana Nasi Kivipi?

7. Tunasasisha Taarifa hii Kivipi?

1. Tunakusanya Data Gani Kukuhusu?

Kama sehemu ya huduma ya AppGallery, tutakusanya na kutumia data yako ya kibinafsi tu kwa malengo yaliyotajwa ndani ya Taarifa hii. Data ya kibinafsi inarejelea maelezo yoyote yanayotuwezesha kukutambua kama mtumiaji.

Tutakusanya na kusindika data ifuatayo:

Maelezo ya akaunti ya Kitambulisho cha HUAWEI, kama vile jina la akaunti (barua pepe au nambari ya simu), picha ya wasifu, jina la utani, tarehe ya kuzaliwa, nchi/eneo, kitambuaji akaunti, na cheti cha huduma cha kitambuaji akaunti.

Maelezo ya kifaa, kama vile kitambuaji kifaa (kama vile SN, UDID, au IMEI, kulingana na toleo la mfumo wa kifaa chako), mipangilio ya lugha, modeli ya kifaa, toleo la mfumo endeshi wa kifaa na toleo la ROM, ukubwa na mwonekano wa skrini, msimbo wa nchi wa simu, na nchi ya ufikishaji.

Maelezo ya mtandao, kama vile anwani ya IP, aina ya mtandao, na hali ya muunganisho wa mtandao.

Maelezo ya matumizi ya huduma, kama vile chanzo cha upakuaji na nambari ya toleo la AppGallery, muda wa matumizi ya programu, nyakati za ubonyezaji na ufichuzi wa programu, historia ya utafutaji ya programu, matokeo na historia ya upakuaji na usakinishaji wa programu, matokeo ya kuingia kwenye programu, maelezo ya programu zilizosakinishwa (kama vile kategoria na toleo), orodha ya programu zilizosakinushwa, kiwango cha pesa cha agizo la ununuzi wa programu, wakati wa agizo, Kitambulisho cha agizo, orodha ya programu zilizosakinishwa, rekodi ya zawadi (tuzo) za mtumiaji, maoni kuhusu programu, rekodi ya kuingia ya makubaliano ya mtumiaji, kitambulisho cha kituo cha matangazo ya programu, kiungo cha kuelekea kwenye ukurasa wa tovuti wa programu, na programu za orodha unayopenda.

Maelezo ya Huduma za Michezo, kama vile Kitambulisho cha Mchezaji, daraja, matimizo, takwimu za wachezaji, na data ya matumizi ya michezo ambayo tunayapokea kutoka kwa mtoaji wa programu ya mchezo unayocheza.

Ukishinda tuzo wakati wa mojawapo kati ya matangazo ya HUAWEI AppGallery, anwani yako ya ufikishaji na nambari ya simu/anwani ya barua pepe zitasindikwa ili kukufikishia tuzo.

Ukitumia HUAWEI AppGallery ndani ya hali ya mgeni (bila ya kuingia ndani kwa kutumia akaunti yako ya Kitambulisho cha Huawei), data ifuatayo itakusanywa na kusindikwa:

Maelezo ya kifaa, kama vile kitambuaji kifaa kama vile SN, UDID au IMEI, kulingana na toleo la mfumo wa kifaa chako, mipangilio ya lugha, aina ya kifaa, toleo la mfumo endeshi wa kifaa na toleo la ROM, ukubwa na mwonekano wa skrini, na nchi ya ufikishaji.

Maelezo ya mtandao, kama vile anwani ya IP, msimbo wa nchi wa simu (MCC), msimbo wa mtandao wa simu (MNC), aina ya mtandao na hali ya muunganisho wa mtandao

Maelezo ya matumizi ya huduma, kama vile nambari ya toleo la AppGallery, wakati wa kufungua na kufunga programu, ufichuzi, historia ya utafutaji wa programu, historia ya upakuaji na usakinishaji wa programu, maelezo ya programu zilizosakinishwa (kama vile kategoria na toleo), orodha ya programu zilizosakinishwa, ripoti za uendeshaji na ripoti za hitilafu, kitambulisho cha kituo cha matangazo ya programu, kiungo cha kuelekea kwenye ukurasa wa tovuti wa programu, na rekodi ya kuingia ya makubaliano ya mtumiaji.

Ili kukupatia huduma zinazohitajika, AppGallery inahitaji vibali ili kufikia simu yako ili kupata maelezo ya kifaa, na hifadhi yako ili kudhibiti mafurushi ya usakinishaji. Pia unaweza kudhibiti vibali ndani ya mipangilio yako ya kifaa.

2. Tunatumia Data Yako Kivipi?

Ili kukupatia huduma za AppGallery na kukidhi majukumu ya kimkataba, tunahitaji kukusanya data yako ya kibinafsi ili uweze kuvinjari, kufikia, kupakua, kudhibiti programu zako, na kujiburudisha na vipengele vinavyohusu michezo. Hii pia inatuwezesha tusindike data yako kwa malengo ya utambulisho, ukamilishaji wa malipo, udhibiti wa uhusiano na wateja, usaidizi na mawasiliano, ushughulikiaji wa malalamishi ya wateja, udumishaji, masasisho ya mfumo, utambuzi na urekebishaji wa tatizo.

Kwa ziada, tunatumia data yako ya kibinafsi kwa malengo yafuatayo baada ya kupokea idhini yako:

Malengo ya uchambuzi na ukuzaji, yakiwemo kuunda vikundi vilivyounganishwa kwa msingi wa shughuli za matumizi za vikundi tofauti vya watumiaji. Hii pia inatuwezesha kuelewa mahitaji ya watumiaji wetu kama wateja na kuimarisha ubora na uzoefu wa mtumiaji wa huduma na vitolewavyo vyetu vya sasa na vya siku zijazo, na pia kutathmini ufanisi wa kampeni na matangazo. Unaweza kupinga usindikaji huu wa data kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.6 hapo chini.

Kuwasiliana kuhusu vitolewavyo vyetu, malengo ya ukuzaji wa mauzo na utafutaji soko na pia kuunda vikundi vinavyolengwa vilivyounganishwa kwa ajili ya utafutaji soko. Kujua wanayoyapenda wateja wetu kunatuwezesha kulenga vitolewavyo vyetu na bidhaa na huduma zetu zitolewazo zinazokidhi kwa ubora zaidi mahitaji na matakwa ya wateja wetu. Unaweza kupinga usindikaji huu wa data kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.6 hapo chini.

Tunaweza kusindika data yako ya kibinafsi kwa ajili ya huduma za kubinafsisha kwa kutoa mapendekezo na kwa kuonyesha programu zinazolengwa ndani ya AppGallery. Unaweza kupinga usindikaji huu wa data kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.6 hapo chini.

Ikiwa umewezesha ubinafsishaji wa Matangazo ya HUAWEI kwenye kifaa chako, kategoria za programu ulizosakinisha (kama vile michezo, mitandao ya kijamii, michezo) zitatumiwa ili kukuonyesha matangazo yanayokuhusu zaidi kwenye HUAWEI Mobile Services na programu za watu wengine zinazotoka kwenye jukwaa la Matangazo ya HUAWEI. Ili kupata maelezo zaidi kuhusu Matangazo ya HUAWEI na kuhusu haki zako, bofya hapa (https://consumer.huawei.com/ minisite/cloudservice/ad/ privacy-statement.htm?country=HK&language=sw-tz).

Malengo ya usalama wa maelezo, yakiwemo kugundua na kuzuia aina mbalimbali za matumizi mabaya ya huduma na udanganyifu ili kukupatia huduma salama na za kuaminika.

Ukiwezesha Huduma za Michezo ndani ya programu ya mchezo ya mtu mwingine, na ikiwa umeidhinisha programu ipate data yako ya Huduma za Michezo (Kitambulisho cha Mchezaji, daraja, matimizo, na takwimu za wachezaji), data yako ya Huduma za Michezo itafichuliwa kwa programu ya mchezo ya mtu mwingine. Unaweza kuondoa idhini hii wakati wowote kwa kuenda kwenye Mipangilio > Kitambulisho cha HUAWEI > Kituo cha faragha > Dhibiti ufikiaji wa akaunti kwenye kifaa chako.

Ukitoa maoni kuhusu programu inayopatikana ndani ya AppGallery, tutafichua maoni yako na jina lako la utani kwa muundaji wa programu ili kusaidia kuboresha huduma kwa msingi wa tathmini na majibu yako.

Unapokuwa unatumia HUAWEI AppGallery huku umeingia ndani kwa kutumia Kitambulisho chako cha HUAWEI, tunaweza kutuma taarifa za msukumo kwa kifaa chako ili kukujulisha kuhusu programu mpya zinazopatikana, matukio na shughuli zinazohusu tuzo, baada ya wewe kutoa idhini ndani ya programu ya AppGallery. Unaweza kuondoa idhini yako wakati wowote kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Mipangilio, na kulemaza Pokea taarifa.

Pia tunaweza kusindika kiwango cha pesa cha agizo la kununua programu, wakati wa agizo na Kitambulisho cha agizo kwa ajili ya malengo ya kodi ya serikali na uhasibu kama inavyotakikana na sheria na kanuni zinazotuhusu.

3. Tunahifadhi Data Yako kwa Muda Gani?

Tutabakisha data yako ya kibinafsi kwa muda usiozidi ule unaohitajika kwa malengo yaliyobainishwa ndani ya Taarifa hii.

Tutasindika na kubakia na data yako kwa kipindi chote cha muda wa uhusiano wako wa kimteja na sisi. Ukifuta akaunti yako ya Kitambulisho cha HUAWEI, data na huduma zote zinazohusishwa na akaunti yako, zikiwemo programu ya AppGallery, zitafutwa. Hata hivyo, tutabakisha:

Kiwango cha pesa cha agizo la ununuzi wa programu, wakati wa agizo na Kitambulisho cha agizo kwa miaka misaba (7) kuanzia tarehe ya kufanywa malipo.

Data ya kibinafsi iliyosindikwa kwa ajili ya udhibiti wa uhusiano na mteja kama vile malalamishi, maombi ya mada ya data na malengo ya udhibiti wa mkataba kwa hadi miaka misita (6) kuanzia mwingiliano wa mwisho.

Data ya kibinafsi inayosindikwa kwa malengo ya kudhibiti mkataba kwa hadi miaka mitatu (3) baada ya Kitambulisho chako cha HUAWEI kufutwa.

Data ya kibinafsi inayosindikwa kwa malengo ya uchambuzi wa kitakwimu na uuundaji bidhaa na pia ukuzaji wa mauzo na utafutaji soko kwa hadi miezi kumi na miwili (12) baada ya tarehe ya kukusanywa, isipokuwa ikiwa unapinga usindikaji huu.

Anwani yako na nambari ya simu/anwani ya barua pepe kwa mwaka mmoja (1) baada ya wewe kutumiwa tuzo.

Hifadhi rudufu na ripoti za programu zinazosindikwa ili kuhakikisha usalama wa data na huduma zako kwa hadi miezi misita (6) kuanzia tarehe ya kuundwa kwao.

Ukilemaza Huduma za Michezo, data yako itaondolewa ndani ya siku thelathini (30) isipokuwa ikiwa kuna misingi husika ya kisheria ya kuendeleza usindikaji wa data kama ilivyofafanuliwa hapo juu. Unapokuwa unatumia huduma ndani ya hali ya mgeni, maelezo yako ya mtandao na maelezo yako ya matumizi yatasindikwa kwa siku saba (7).

Pindi kipindi cha muda wa kubakisha kinapoisha, tutafuta na kuondolea majina data yako ya kibinafsi, isipokuwa ikiwa inahitajika kivingine na sheria na kanuni husika.

4. Tunagawiza Data Yako Kivipi?

Tunahifadhi data yako ndani ya vituo vya data vilivyoko ndani ya Hong Kong (Uchina) na Singapoo.

Shughuli zetu za udumishaji zinaweza kutuhitaji kufikia data yako kutoka India na Uchina. Kwa ziada, data yako pia inaweza kusindikwa na vituo vyetu vya huduma kwa wateja vilivyoko, kwa mfano, ndani ya Meksiko, Misri, Afrika Kusini, Saudi Arabia, Pakistani, Myama, India na Malesia, kulingana na eneo lako.

Tunagawiza data yako tu:

Unapotoa maoni kuhusu programu inayopatikana ndani ya AppGallery, maoni yako, jina la utani, modeli ya kifaa na wakati ambao maoni hayo yalitolewa yatafichuliwa kwa muundaji wa programu ili kuboresha huduma yao na/au kurekebisha matatizo.

Unapowezesha Huduma za Michezo na kuidhinisha programu ya mchezo ya mtu mwingine isindike maelezo yako ya Huduma za Michezo, daraja, matimizo, ununuzi, na takwimu za wachezaji zitafichuliwa kwa programu ya mchezo ya mtu mwingine ili kukupatia vipengele vya michezo na kuboresha uzoefu wako wa michezo.

Unapochagua kuhifadhi data yako ya Huduma za Michezo kwenye Cloud yako, na unapokuwa umebadilisha nchi/eneo la huduma ndani ya AppGallery, data ndani ya mchezo uliyohifadhi kisha huenda ikafichuliwa kwa kampuni zingine zinazomilikiwa na Huawei, ambazo zinakupatia huduma za Cloud na ziko ndani ya Uchina au Ayalandi (https://cloud.huawei.com/privacyStatementTransit), kulingana na nchi/eneo lako la usajili wa Kitambulisho cha HUAWEI.

Inapohitajika ili kujibu mchakato au ombi la kisheria kutoka kwa mamlaka adilifu kulingana na sheria husika au kuhusiana na kesi au mchakato wa kisheria.

Inapohitajika kama sehemu ya muunganisho wa kampuni, ununuzi wa kampuni, uuzaji wa mali (kama vile makubaliano ya huduma) au mpito wa huduma hadi kwa kikundi cha Huawei au kampuni nyingine.

5. Una Haki Zipi na Machaguo Yapi?

Una haki na machaguo yafuatayo:

5.1 Kufikia data yako

Unaweza kuwasilisha ombi la nakala na ufafanuzi wa data yako ya kibinafsi ambayo tumeikusanya na kuihifadhi kuhusiana na AppGallery kwa kuenda kwenye Mipangilio > Kitambulisho cha HUAWEI > Kituo cha faragha > Agiza data yako, kwenye kifaa chako.

Ili kutuma ombi la ziada la ufikiaji, ikiwemo kuitisha nakala ya data yako unapokuwa unatumia AppGallery ndani ya hali ya mgeni, tafadhali wasiliana nasi (https://consumer.huawei.com/ uk/legal/privacy-questions).

5.2 Kusahihisha data yako

Ili kuhifadhi data yako iwe ni ya hivi karibuni na ni sahihi, unaweza kufikia na kurekebisha data yako kwa kuenda kwenye Mipangilio > Kitambulisho cha HUAWEI.

Unaweza kufikia na kubadili maelezo yako ya ufikishaji kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Mipangilio > Maelezo ya ufikishaji.

5.3 Kuhamisha data yako

Unaweza kuhamisha data ya kibinafsi ambayo umetupatia kuhusiana na AppGallery ndani ya umbizo litumikalo sana na linaloweza kusomwa na mashine kwa kuenda kwenye Mipangilio > Kitambulisho cha HUAWEI > Kituo cha faragha > Agiza data yako, kwenye kifaa chako.

Pia unaweza kuhamisha data yako ya kibinafsi ambayo umetupatia ndani ya AppGallery, unapokuwa unatumia huduma ndani ya hali ya mgeni, ndani ya umbizo litumikalo sana na linaloweza kusomwa, kwa kuwasiliana nasi.

5.4 Kufuta data yako

Wakati wowote unaweza:

Kufuta historia yako ya upakuaji na usakinishaji wa programu, na rekodi za ununuzi kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Historia ya ununuzi.

Kufuta rekodi zako za tuzo kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Tuzo.

Kufuta programu zilizoko ndani ya orodha unayoipenda kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Orodha unayopenda.

Kufuta maelezo yako ya ufikishaji kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Mipangilio > Maelezo ya ufikishaji.

Kufuta akaunti yako ya Kitambulisho cha HUAWEI. Kutokana na hayo, data yako yote ya kibinafsi na huduma zote zinazohusiana na akaunti yako ya Kitambulisho cha HUAWEI zitafutwa, zikiwemo data yako ya kibinafsi ndani ya AppGallery.

Kupinga usindikaji wa data yako kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 5.6. Ikiwa kupinga kwako ni halali, na hatuna msingi wowote wa kisheria wa kuendelea kusindika data yako, tutafuta data husika ndani ya upana wa upingaji wako wenye ufanisi.

Kuwasiliana nasi (https://consumer.huawei.com/ uk/legal/privacy-questions) ikiwa unadhani kuwa usindikaji wa data yako ya kibinafsi unakiuka sheria na data yako inafaa kufutwa.

Tutafuta au kuondolea majina data yako ya kibinafsi ndani ya kipindi cha muda kinachoeleweka kulingana na hatua zilizotajwa hapo juu na kulingana na vipindi vya kubakishwa kama ilivyoelezwa ndani ya Kifungu cha 3.

5.5 Kuondoa idhini yako

Ikiwa umechagua kupokea utafutaji soko wa elektroniki wa moja kwa moja kutoka kwetu, unaweza kuondoa idhini yako kwa kuenda kwenye AppGallery > Mimi > Mipangilio, na kulemaza Pokea taarifa.

Ikiwa umeidhinisha programu za michezo za watu wengine zipokee maelezo yako ya Huduma za Michezo, unaweza kuondoa idhini yako kwa kuenda kwenye Mipangilio > Kitambulisho cha HUAWEI > Kituo cha faragha > Dhibiti ufikiaji wa akaunti.

5.6 Kupinga usindikaji

Ikiwa unataka kupinga usindikaji wa data yako kwa malengo ya uchambuzi, mapendekezo, uendelezaji, mauzo na utafutaji soko, tafadhali wasiliana nasi (https://consumer.huawei.com/ uk/legal/privacy-questions).

Unapowasilisha ombi, tafadhali bainisha upana wa ombi na tupatie anwani yako ya barua pepe au nambari ya simu uliyoitumia kuingia ndani kwenye Kitambulisho chako cha HUAWEI, ikiwa ulitumia huduma ndani ya hali ya umeingia ndani, au kitambuaji kifaa chako ikiwa umekuwa ukitumia AppGallery ndani ya hali ya mgeni.

Tutawasiliana na wewe ili kuthibitisha utambulisho wako ili kuendelea na ombi lako.

5.7 Kuzuia usindikaji

Ikiwa unataka kuzuia usindikaji wa data yako ya kibinafsi, tafadhali wasiliana nasi (https://consumer.huawei.com/ uk/legal/privacy-questions). Una haki ya kuzuia usindikaji wa data yako kwenye hali zifuatazo:

Data yako inasindikwa kwa njia isiyo halali, lakini hutaki kuifuta.

Una dai la kisheria ambalo unahitaji kuliimarisha, kulitumia na kulilinda, na ulituomba tuhifadhi data yako ambapo hatungeihifadhi kivingine.

Umekana usahihi wa data yako ya kibinafsi na usahihi wa data yako unasubiri uthibitishaji wetu.

Ombi lako la kupinga itabidi lisubiri taratibu yetu ya uthibitishaji.

Unapowasilisha ombi, tafadhali bainisha upana na misingi ya ombi hilo na tupatie anwani yako ya barua pepe au nambari yako ya simu uliyotumia kuingia ndani kwenye Kitambulisho chako cha HUAWEI.

Tutawasiliana na wewe ili kuthibitisha utambulisho wako ili kuendelea na ombi lako.

6. Utawasiliana Nasi Kivipi?

Unaweza kupata mwongozo wa jinsi ya kutumia haki zako za mada ya data ndani ya Kifungu cha 5. Ikiwa una maswali, maoni, au mapendekezo yoyote kuhusu haki zako kama mada ya data au usindikaji wetu wa data yako ya kibinafsi au ikiwa unataka kuwasiliana na Afisa wetu wa Ulinzi wa Data, tafadhali wasiliana nasi (https://consumer.huawei.com/ uk/legal/privacy-questions).

Anwani ya makao yetu makuu: Huawei Services (Hong Kong) Co., Limited, Chumba cha 03, 9/F, Mnara wa 6, The Gateway, Namb. ya 9 Barabara ya Kantoni, Tsim Sha Tsui, Kowloon, Hong Kong. Nambari ya usajili 1451551.

Ikiwa unaamini kuwa hatusindiki data yako ya kibinafsi kulingana na Taarifa hii au sheria husika za kulinda data, unaweza kutuma lalamishi kwa mamlaka ya ulinzi wa data ndani ya nchi/eneo lako, au Kamishna wa Faragha wa Data ya Kibinafsi ndani ya Hong Kong.

7. Tunasasisha Taarifa hii Kivipi?

Tunakuhimiza uangalie mara kwa mara toleo la hivi karibuni la Taarifa hii ndani ya mipangilio ya programu kwani tunaweza kuisasisha mbeleni. Kunapotokea tukio la mabadiliko marudufu kwenye Taarifa hii, tutakuarifu mapema kwa kutumia visanduku vya taarifa, ujumbe wa msukumo, barua pepe, na kadhalika, kulingana na hali ya badiliko.

Onyeshazaidi